Kama ulipata nafasi ya kutizama mchezo wa Brazil na Bolivia ulipigwa alhamisi ya Septemba, 6 utakuwa na ufahamu mzuri kuhusu tukio lililompata kwa mchezaji wa Brazil, Neymar kwa kupigwa kiwiko na beki wa Bolivia, Yasmani Duk.
Baada ya Duk kumpiga kiwiko Neymar, Neymar alipasuka katika paji la uso na kuanza kutokwa na damu lakini katika hali ambayo imewashangaza watu wengi ni Duk kukataa kumuomba msamaha Neymar.
Duk amesema kilichotokea ni hali ya kawaida katika mchezo kwani mchezo huo ni wa nguvu na yeye alikuwa akijaribu kumzuia Neymar ili asiende kusababisha madhara katika lango lao na hivyo haoni haja ya kuomba msamaha kwani hata yeye amewahi kuvunjika pua na hakuna mtu aliyezungumza.
“Nilichojaribu kufanya ni kumzuia, jambo ambalo huwa linatokea katika mchezo wa soka, kila mtu anajua huu mchezo ni wa kutumia nguvu, mimi pua yangu iliwahi kuvunjika na hakuna aliyezungumza,
“Kuwa mchezaji bora duniani, anatakiwa kuacha tabia za ‘Charlie Big Boll****’ na kuanza kuonyesha heshima kwa wapinzani wake,” amesema Duk.