,

,

,

,
Entertainment

Mr T Touch athibitisha kumsaini Young Dee kwenye lebo yake

Mr T Touch amethibitisha kumsajili Young Dee kwenye lebo yake, Touchez Sound Records kwa miaka mitatu.
Mtayarishaji huyo wa muziki amekiambia kipindi cha E-News cha EATV Ijumaa hii kuwa yeye atakuwa anasimamia kutengeneza beat za nyimbo zote za msanii huyo.
“Mimi nimeingia mkataba mrefu wa miaka mitatu na Young Dee. Ataendelea kuwepo chini ya Touchez Sound na mimi ndiye nitakayesimamia na kutengeneza beat za nyimbo zake zote. Nia yangu ni kumfanya afanye vitu tofauti na alivyokuwa akifanya hapo awali kwa kuwa mimi namuona ni msanii mwenye biashara,” amesema Touch.
Young Dee alikuwa anasimamiwa kazi zake na MDB ya Max Rioba kabla ya kutangaza kuachana naye mapema mwanzoni mwa mwaka huu.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.