,

,

,

,
Sports

Yanga yakubali kipigo kutoka kwa Ruvu Shooting

Mchezo wa kirafiki baina ya klabu ya Dar es salaam Young Africans dhidi ya Ruvu Shooting umemalizika kwa bingwa huyo wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara kukubali kipigo cha goli 1-0 katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Yanga SC inapoteza mchezo huo wa kirafiki ikiwa imesalia wiki moja na siku kadhaa kuchezwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya wapinzani wao wajadi Simba SC Agosti 23 mwaka huu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara.
Ruvu imetoka kifuambele katika mchezo huo kwa bao pekee lililofungwa na beki wa Yanga, Ally Shaibu ‘Ninja’ katikadakika ya 22.
Safu ya ushambuliaji ya Yanga ilijitahidi kuhakikisha wanarudisha bao hilo katika kipidi chote cha mchezo lakini juhudi zao hazikuzaa matunda na hivyo mpira kumalizika kwa ushindi huo mwembamba kwa vijana wa Masau Bwire.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.