,

,

,

,
Music

Amini Amrushia Dongo Linah Sanga...Adai Nyimbo zake za Sasa Sio Nzuri Zinakosa Uyeye....

Amini aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Linah uliodumu kwa miaka mingi kabla ya kuachana na kila mmoja akawa na maisha yake.


Pia Amini aliwahi kumwandikia msanii huyo nyimbo kadhaa zilizofanya vizuri. Lakini sasa hitmaker huyo wa ‘Bado Robo Saa’ amesema kuwa Linah wa sasa si yule wa zamani katika uimbaji.


“Linah wa sasa anakosa uyeye aliokuwa nao mwanzo wakati mimi namuandikia nyimbo,” Amini alimwambia mtangazaji wa Kings FM, Prince Ramalove.

“So nyimbo anazozipata sasa hivi sio nyimbo za kuimba yeye. Nafikiri pia mwandishi anayemuandikia bado hajamjulia jinsi ya kumwandikia nyimbo za aina gani au idea ya aina gani, vile vile studio anazorekodia au producer anayerekodi naye anakuwa hajamjulia,” aliongeza.

Amini anasema bado ana uwezo wa kumwandikia Linah kwakuwa ni kwake ni sehemu ya biashara

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.