Kama
ilivyo kawaida ya kila kiongozi kuwa na namna yake ya uendeshaji wa
madaraka ambayo anakuwa amepatiwa, hivyo ndivyo ilivyo kwa Rais wa FIFA,
Gianni Infantino ambaye katika awamu yake anataka kufanya mabadiliko
kwa kuongeza timu ambazo zinashiriki Kombe la Dunia.
Akiwa
katika ziara Bogata, Colombia, Infantino alisema ametoa mapendekezo kwa
Baraza la FIFA kutaka kuongeza idadi ya timu ambao zitakuwa zinashiriki
Kombe la Dunia lakini zitakuwa zinafanyiwa mchujo na kubakiza timu 32,
pendekezo ambalo linataraji kujadiliwa wiki ijayo na kutolewa maamuzi
mwezi Januari, 2017.
Alisema
mfumo huo mpya utapitisha timu 16 moja kwa moja kushiriki mashindano na
zingine 32 zitacheza zenyewe kwa zenyewe na baada ya hapo timu 16
zitaungana na nyingine 16 ambazo zimeshafuzu na ndipo zitaingia katika
hatua ya makundi.
“Wazo
langu ni timu 16 zitafuzu hatua ya makundi na 32 zitashindana kutafuta
timu zingine za kufuzu, watacheza katika nch ambayo Kombe la Dunia
litakuwa linachezwa, watacheza kutafuta nafasi 16 zilizosalia,
“Ina
maana tutaendelea na mfumo wa kawaida wa timu 32 kushiriki Kombe la
Dunia, lakini timu 48 zitahusika na mashindano,” alisema Rais wa FIFA,
Infantino.
Aidha
mtandao wa Reuters umeripoti kuwa, pendekezo ambalo amelitoa Infantino
linakubalika na Baraza la FIFA na kinachosubiriwa ni muda ufike ili
maamuzi yatangazwe
0 comments:
Post a Comment