Idadi ya vifo kufuatia kimbunga Matthew nchini Haiti inakaribia watu 300, kwa mujibu wa serikali.
Katika Mji wa Jeremie asilimia 80 ya majengo yameporomoka.Hadhi ya Kimbunga Matthew kwa mara nyingine imepandishwa hadi ngazi ya nne, hatua ambayo ndiyo ya pili kwa ukubwa katika mgawanyo wa aina mbali mbali za Kimbunga, huku kikielekea katika jimbo la Florida nchini Marekani.
- Vimbunga vinavyopewa majina duniani
Siku ya alhamisi, serikali ya nchi hiyo ilisema watu mia moja tayari walikuwa wamepoteza maisha yao.
Kimbunga Matthew ambacho ndicho kubwa zaidi katika visiwa vya Caribbean kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, kimepiga taifa la Bahamas baada ya kupitia Haiti na Cuba.
Wengi wa waliopoteza maisha nchini Haiti, walikuwa wakiishi mjini na vijiji vinavyojulikana kwa shughuli za uvuvi katika maeneo ya pwani ya kusini.
- Obama atangaza hali ya hatari Florida
Kimbunga hicho kiliambatana na upepo uliokuwa ukivuma kwa kasi ya hadi kilomita 280 kwa saa
Usafiri kati ya maeneo ya kusini Magharibi na meneo mengine nchini Haiti ulisitishwa baada ya daraja moja muhimu inayounganisha maeneo hayo kusomba na maji.
Mashirika yasiyo ya kiserikali yamesema kwa sasa hakuna huduma za simu na umeme na kuwa watu wanapungukiwa na vyakula na maji safi ya kunywa.
SOURCE: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment