Zaidi ya wanajeshi 20 wameuawa
katika kambi inayotumiwa na wakimbizi wa Mali nchini Niger. Maafisa
wanasema shambulio hilo limetekelezwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu.
Waziri Mkuu Brigi Rafini aliiambia televisheni ya taifa kuwa shambulio hilo lilitokea ukanda wa magharibi wa mkoa wa Tahoua.Waasi walilenga eneo lililopo karibu na kambi ya jeshi.
Ukanda wa magharibi na kati wa taifa la Mali umekuwa hauko salama kwa kipindi cha miaka minne sasa tangu ufaransa ilipoingilia kati jitihada za kuwaondoa wapiganaji wa Jihadi.
Mapigano ya Niger yamekuwa tishio kwa pande zote tatu ,askari walijeruhiwa katika shambulio hilo,Maofisa wa eneo hilo wamesema yawezekana vifo vikaongezeka.
Mwezi uliopita ,wakimbizi wawili waliuwawa na watu wenye silaha wasiofahamika wakati walipovamia eneo la usalama lililopo katika kambi za Tabarey barey nchini Niger,ambapo pia kulikuwa na nyumba za wakimbizi wa Mali.
Jeshi la Niger sasa linapigana na wanamgambo wa kiislam wa boko haram wanaotaka kuingia kwenye mipaka ya kusini mwa Nigeria pamoja na kujaribu kuzuia vurugu zinazoweza kuenea kutoka Mali mpaka Magharibi.
0 comments:
Post a Comment