,

,

,

,
Entertainment

Ukosefu wa Elimu kwa Bongo Movie ndo Chanzo Kikubwa cha Tasnia Hiyo Kushuka- Shamsa Ford

Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amewaponda baadhi ya wasanii wa Bongo movie na kusema ukosefu wa elimu kati yao chanzo kikubwa tasnia hiyo kushindwa kuendelea na kupiga hatua kubwa na kudai wamekalia umbea, chuki, ushirikina na roho mbaya.
"Mama yangu alinikazania sana nisome kwa bidii wakati nipo shule ila nilipomaliza form 6 nikaona inatosha. COUNTER BOOK la shule nikaona zito ila SCRIPT ya movie nikaona jepesi..Natamani ningerudisha siku nyuma ningesoma kwa bidii hata kama ningetaka kuwa muigizaji basi ningekuwa muigizaji wa kimataifa mwenye maarifa. Moja ya vitu vikubwa vinavyoturudisha nyuma bongo movie ni elimu. Mtu aliyesoma na asiyesoma ni vitu viwili tofauti. sasa sisi wenge wetu hatuna elimu kabisaa" aliandika Shamsa Ford
aliendelea kusisitiza kuwa "wengi wao darasa 7,5,2,6 wengine ndiyo kabisaa alijifunza kusoma na kuandika tu. Nakumbuka mwaka juzi nilimuona msanii wa Nigeria Genevieve akiojiwa CNN nikatamani niwe mimi. Wenzetu wamesoma ndiyomaana wametupita vitu vingi sana. Huku bongo movie kumejaa umbea, chuki, roho mbaya, ushirikina, mtu hata kama hujawahi kumkosea lakini akikaa na watu wanaokuchukia atakusema vibaya, Lakini pia ukijitenga useme uishi kivyako utaambiwa unalinga na vikao utaekewa. Yote haya ni kwasababu ya ukosefu wa elimu ndomaana watu wanaweza kupoteza muda kwa vitu vya kijinga" alisisitiza Shamsa Ford

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.