,

,

,

,
Sports

Pochettino ammwagia sifa Paulo Gazzaniga baada ya ushindi dhidi ya Crystal Palace

Meneja wa klabu ya Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino amemmwagia sifa mlinda lango wa timu hiyo raia wa Argentina, Paulo Gazzaniga baada ya kuchomoza na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace.

Spurs ikiwa nyumbani Uwanja wa Wembley ilichomoza na ushindi huo kupitia bao safi la mshambuliaji wa kimataifa wa Korea Kusini, Son Heung-Min dakika 64 ya mchezo na kupelekea matokeo kumalizika kwa ushindi huo.
Kufuatia kiwango bora kilichoonyeshwa na mlindalango wa Spurs, Paulo Gazzaniga  katika harakati za kuokoa michomo kadhaa iliyokuwa ikilenga lango lake meneja wa kikosi hicho, Pochettino amesema nikiwango bora kabi kilichoonyeshwa na kipa wake.

“Najiskia furaha kwa wachezaji mbalimbali wanao jiunga na timu hii, watu kama Paulo wamecheza vizuri sana,” amesema Pochettino.
Pochettino ameongeza “Hili huwezi kuamini kwakuwa na kipa kama huyu kwa hakika najisikia furaha kwake na wenzake aliyocheza nao.”
“Ulikuwa mchezo mgumu kwetu Palace walikuwa mara kwamara wanatushambulia na kucheza pasi ndefu tulicheza ila hatukupata nafasi nyingi.”
“Wamekuwa vizuri baada ya kufanya maandalizi ya wiki moja, tulikuwa na matatizo machache baada ya mchezo wetu na Madrid na ndiyomaana naufurahia ushindi huu na kkwa kupata pointi  hizi tatu.”
Kikosi cha Tottenham kilichocheza ni Gazzaniga (9), Aurier (6), Sanchez (8), Vertonghen (8), Rose (8), Dier (7), Winks (6), Sissoko (6), Eriksen (6), Son (7), Kane (6)
Wachezaji wa hakiba Davies (6), Dembele (6), Llorente (6)
Kwa upande wa Palace ni Speroni (7), Ward (6), Dann (8), Sakho (8), Fosu-Mensah (6), Loftus-Cheek (6), Cabaye (6), Milivojevic (6), Schlupp (6), Townsend (8), Zaha (8)
Wa hakiba Sako (6)
Aliyeibuka mchezaji bora wa mchezo huo ni mlinda lango wa Spurs, Paulo Gazzaniga
Katika mchezo huo mfungaji goli wa Spurs ambaye ni mshambuliaji wa timu ya Korea Kusini, Son Heung-Min ameweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka bara la Asia kuwa na mabao mengi zaidi katika ligi kuu ya Uingereza.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.