,

,

,

,
AFYA

Fahamu kuhusu msongo wa mawazo

Watalamu wa masuala ya saikolojia wanasema ya kuwa kila binadamu, huwa na msongo wa mawazo, hii ni kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha ikiwemo na changamoto za kimahusiano, na mambo mengine mengi.

Athari zitokanazo ni kuwepo kwa mawazo katika akili ya mwanadamu ni kama ifuatavyo;-
1. Kuwa na mawazo hisababisha mwili kuwa dhoofu, pia muda mwingine kuweza kusabaisha magonjwa mengine.
2. Kuoatwa magonjwa ya shinikizo la moyo, ni sababu tosha kwamba chanzo chake ni msongo wa mawazo.
3.Kuharibika kwa nywele ikiwa ni pamoja na kukatika kwa nywele hivyo unapoona nywele zako hazikui vyema wakati unazihudumia vizuri tatizo huweza kuwa ni hilo la msongo wa mawazo pia.
4. Akili kushindwa kufanya kazi vizuri.
Njia za kuondoa msongo wa mawazo:
1.  Kukwepa vyanzo vya msongo wa mawazo:- Usipende kukaa na wanaokusababaishia ama kukupa msongo wa mawazo, tafuta mazingira mengine tofauti na hayo.
2.  Badilisha mazingira:- Hii inaweza kukusaidia kwani itaupa nafasi ubongo wako kufikiri mawazo mengine mapya. Wengine hupendelea kutembelea sehemu tofauti kama kusafiri.
3.  Pumzisha na burudisha mwili wako:- Unaweza kupumzisha mwili kwa kusikiliza muziki ama kuangalia vipindi vya kukuburudisha mfano vichekeosho.
4. Mazoezi na chakula kizuri:- Hakikisha unapata chakula kizuri na kinachokupendeza (unachokipenda) ila zingatia mlo kamili na pendelea kufanya mazoezi  mepesi.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.