,

,

,

,
Entertainment

Bongo Dar es Salaam ilitaka kunifilisi – Dude

Dude amedai kuwa kipindi chake cha Bongo Dar es Salaam kilichokuwa kikiruka kupitia TBC One, kilikaribia kumfilisi.

Amedai kuwa alikuwa akitumia gharama kubwa kukiandaa lakini malipo aliyokuwa akipokea kutoka kwenye kituo hicho ni madafu. Muigizaji huyo ambaye jina lake halisi ni Kulwa Kikumba amesema hiyo ndio sababu iliyomfanya akiondoe kipindi hicho.
“Nilikua naandaa kipindi kwa gharama kubwa mno halafu faida nikawa napata ndogo kwahiyo kiuchumi nikawa nayumba nashindwa hata kuandaa vipindi,” Dude alikiambia kipindi cha Kaseti cha Kiss FM.
Amedai kuwa ukosefu wa wadhamini kwenye kipindi ulikuwa chanzo kingine cha kusitisha kipindi hicho. Hata hivyo amesema anatarajia kukirudisha tena kipindi hicho baada ya kuwepo maombi mengi kutoka kwa mashabiki

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.