,

,

,

,
Gossip

Majibu ya Chris Brown Kuhusu Kumvunjia Simu Shabiki Airport Mombasa

Mwimbaji staa kutoka Marekani Chris Brown October 8 2016 aliungana na wasanii wengine akiwemo Wizkid wa Nigeria, Vanessa Mdee, Alikiba na wengineo kutumbuiza kwenye tamasha la Mombasa Rocks Music Festival lililofanyika  Golf Club Mombasa.


Iliripotiwa kuwa staa huyo kuwa na tuhuma za kumvunjia shabiki Brenda Chepkoech simu alipowasili Airport Mombasa ambae alikuwa katika harakati za kutaka kupiga nae selfie, leo Oct 14 2016 kituo kikubwa cha habari cha Kenya, eDaily kimeripoti majibu aliyatoa Chris brown kuhusu tuhuma hizo na hiki ndicho alichokiongea staa huyo…


”Brenda Chepkoech aliyenipa tuhuma za kumvunjia simu yake oct 8 2016 alikuwa anataka free tickets ili aweze kufika kwenye show hiyo’ – Chris Brown

Imeripotiwa kuwa dada huyo alikua anawafata Chris Brown na kundi zima kuomba ticket na kutaka kupiga selfie na staa huyo lakini ombi lake halikusikilizwa, chris aliwambia marafiki zake…
’ Hata picha inaonyesha sikumsogelea dada huyo wala simu yake, Hapana sio uongo mwingine kuhusu mimi tafadhali’– Chris Brown

Mmoja waandaji wa show hiyo Thandie Ojeer alihojiwa na edaily na haya ndio aliyoyazungumza…

’ Chris hakuwa na hasira kabisa, ilikuwa mara yake ya kwanza kufika Kenya na ame enjoy kuwepo Kenya, pia ameahidi kurudi siku moja na kukaa zaidi na kufanya tour next time– Thandie Ojeer

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.