,

,

,

,
Gossip

Meneja wa Alikiba Afunguka Mkasa Mzima wa AliKiba Kushushwa Stejini Ghafla Huko Mombasa.

American Superstar Chris Brown, Jumamosi ya juzi ali rock kwenye tamasha la Mombasa Rocks Festival, ambalo tamasha hilo lilifanyika kwenye hoteli kubwa inayoitwa Mombasa Golf Hotel.

Mombasa Rock Festival lilikuwa na wasanii wengi wa ku-perform kutoka ndani na nje ya Kenya. Kutoka Bongo tuliwakilishwa na King Kiba pamoja na Vee Money.

Lakini kuna video zinasambaa zikionesha kuwa wakati anaperform Kwenye tamasha hilo, Kiba alipanda juu ya speaker, alitumbuiza nyimbo mbili tu kabla ya mic aliyokuwa anaitumia kuonekana kupata mushkeli/kuzimwa na kumlazimu kuondoka jukwaani na kupandishwa Chris Brown.

Swali..Je kupanda juu ya speaker ndio kulisababisha waandaaji wamshushe Kiba au ?

Kupitia perfect255 ikaona isiwe kesi.. nakumvutia waya moja kwa moja Meneja wa AliKiba, Aidan Charlie nakufunguka haya.

“Hapana kwanza Ilo la kupanda juu ya speaker haikuwa sababu, kwa sababu Wizkid nilimuona pia alipanda na hakushushwa.” aliendelea Aidan

“Issue kubwa iliyokuepo nitime, show ilitakiwa ianze saa 8 mchana na kumalizika usiku kama saa 6 lakini kutokana na wenyewe maorganizer walivyojiorganize mambo haya kwenda kama yalivyopangwa, kwa hiyo baada ya kuanza show saa 8 ikaanza saa 3 usiku.”

“But the time show inaanza wakaperform Navio, Vanessa hata nazizi akaondolewa..” alisema Meneja Aidan.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.