,

,

,

,
Sports

Simba na Yanga zapigwa marufuku na serikali kuutumia uwanja wa Taifa

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ametembelea Uwanja taifa Jumapili hii na kuzipiga marufuku mechi zote za Yanga na Simba kufanyikia uwanjani hapo kutokana na uharibifu wa mageti na viti uliojitokeza siku ya jana katika mechi hiyo ya watani hao wa jadi
Mashabiki wa Simba wakitawanywa kwa mabomu ya machozi hapo jana baada ya kufanya uharibufu wa viti


Pia Nape amezuia mapato ya timu hizo ya mchezo wa jana kutokana na uharibifu huo.
“Simba na Yanga hawatoutumia tena uwanja huu mpaka pale Serikali itakapoona kuwa mazingira yanaruhusu,” alisema Nape. alisema Nape.
Amri hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya mashabiki wa klabu ya Simba, kung’oa viti vilivyopo kwenye majukwaa ya uwanja huo kwa kile walichokidai kupinga uamuzi wa Refa, Martin Saanya aliyechezesha mechi hiyo. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.