,

,

,

,
Gossip

Tetesi za Hemed PHD Kutoka Kimapenzi na Mwigizaji Tausi...Tausi Afunguka

Tetesi za Hemedi PHD kutoka kimapenzi na Tausi... Mwigizaji Tausi afunguka
Muigizaji na mchekeshaji kwenye tasnia ya Bongo Movie, Tausi, amesema hana mahusiano yeyote nje ya kazi na Hemed PHD huku akisema huwa wanakutana kambini na hana hata namba ya simu ya msanii huyo.

Tausi ameibuka na kusema hivyo baada ya kuwepo uvumi wa kujimwaga na staa huyo ambapo aliiambia eNewz “Hemedy ni msanii mwenzangu tu na nilipokuwa nyumbani nilikuwa namuona tu kwenye TV na mara ya kwanza nilipokutanishwa naye na meneja wangu Lamata ilikuwa ngumu hata kuongea naye na nilitetemeka saana na nilikuwa mwoga saana”

Mbali na hilo, Tausi, alizungumza kuhusiana na wavulana ambao wamekuwa wakitamani kuwa naye huku wakijiuliza wataishi vipi na yeye akisema hakuna jambo ambalo haliwezekani kwani hata yeye ana ndoto za kuishi na mwanaume na kuwa na watoto wasiopungua 12.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.