Malkia wa filamu Wastara Juma baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha CCM (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma, amerudiana na mpenzi wake wa zamani, Bond Bin Sinan
Mwigizaji huyo amesema Bond Bin Sinan alikiri makosa yake kwenye vyombo vya habari ndio maana imekuwa rahisi kwake kumsamehe na kurudiana naye.
“Makosa yake aliyokuwa ameyafanya mwanzo ndiyo yaliyosababisha tukaachana nikaamua kuolewa na mtu mwingine,” Wastara alikiambia kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM. “Kwa hiyo baada ya mimi kuachana na aliyekuwa mume wangu na yeye bado alikuwa ananihitaji, nikaona nimkubalie kwa sababu tayari tulikuwa tunafahamiana naye,”
Bond Bin Sinan ni mwigizaji na pia ni director wa filamu
0 comments:
Post a Comment