,

,

,

,
Siasa

Lusinde awakosoa wabunge wanaobeza utendaji Rais Magufuli

Mbunge wa Mtera,Livingstone Lusinde, amesema hajapendezwa na baadhi ya wabunge kukosoa utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli pamoja na watendaji wake

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo Alhamisi hii bungeni mjini Dodoma huku akiwapa msamiati wabunge na kwa kusema ni bora mtu ufe mawazo yabaki hai kuliko mtu uwe hai mawazo yako yamekufa.
“Lakini leo nataka nitamke kwenye bunge hili, rais anafanya kazi nzuri sana na endelee kuifanya bahati nzuri tumekuwa na rais kama mbunge mwenzetu tumekaa nae miaka 20, anatujua wabunge, anaijua nchi, anajua namna tunatabia za kuzusha, hawezi kubabaishwa na maneno yanayotoka humo,tumekuwa na malalamiko katika nchi yetu miaka mingi sana kwamba serikali yetu inalindana mtu anaharibu hapa ana hamishiwa hapa, amekuja rais wa mabadiliko ukiharibu unakwenda, lakini ndugu zangu naomba niwaambie hakuna mtu aneshindwa kumshauri rais,”alisema Lusinde.
“Mimi naomba niwapongeze wabunge wa chama pinzani,nawapongeza kwasababu wamejitoa muhanga wanaposimama kusema serikali imefilisika msifikiri wanaisema serikali hapana wanasehemu wanayolenga,kwasababu ili ujue huyu mtu amefilisika lazimakuwe na vielelezo cha kwanza ashindwe kulipa madeni mtu akishindwa kulipa madeni ujue amefilisika, kwahiyo wabunge pinzani acheni uoga,baada ya kusema setrikali imefilisika,serikali inayokulipeni nyie,serikali inayosomesha watoto bure tamkeni kwamba Mbowe umefilisika umeshindwa kulipa madeni huna sababu ya kuzunguka zunguka unapiga kona,”alieleza.
“Lakini nichukue fursa hii kumpongeza rais wetu kachagua wakuu wa mikoa wote wazuri, wa kwanza Mrisho Gambo, wapili mkuu wa mkoa wa Dodoma,watatu mkuu wa mkoa wa Mwanza, rais anawajua watu wake,big up sana Dkt Magufuli endelea kufanya kazi na tunakuombea,waheshimiwa wabunge naomba niwape msamiati mgumu sana ni bora mtu ufe mawazo yako yabaki hai, kuliko mtu uwe hai mawazo yako yawe yamekufa ujue wewe umepote kabisa hatuwezi kuogopa kuuliza maswali,”aliongeza.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.