,

,

,

,
News

Ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kumbaka mjukuu wake

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilayani Nzega mkoani Tabora, imemhukumu kifungo cha maisha Hubasha Ngasa (62) mkazi wa Kijiji cha Ngonho baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka minne.

Awali Mwendesha Mashtaka wa Jeshi la Polisi, Melito Ukongoji, aliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa la kumbaka mtoto huyo Aprili 24 mwaka 2016 baada ya kuachwa na wazazi wake walipokwenda shambani kulima.
Ukongoji alisema, “Baada ya muda wazazi wa mtoto huyo wakiwa shambani walisikia kelele za mtoto na walipokwenda kuangalia nini kimetokea, walikuta tayari mshtakiwa amembaka na kumjeruhi sehemu zake za siri.”
Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Serafina Nsana, alisema adhabu hiyo imetolewa baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliowasilisishwa na upande wa mashtaka

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.