Kama utamuuliza Mose Iyobo kama atakuja kuwa muimbaji tegemea kusikia jibu la hapana. Dancer huyo maarufu wa Diamond kuwa hana mpango huo bali ataendelea na kazi yake anayoifanya sasa hivi.
Akiongea na gazeti la Dimba, Iyobo amesema hana mpango huo kwa kuwa kuimba kunahitaji akili nyingi ili ufanikiwe kwahiyo kwa upande wake hataweza kufanya hivyo bora aendelee na kazi yake anayoifanya sasa.
“Unajua kuimba kunahitaji akili nyingi ili ufanikiwe, sasa kwa upande wangu sitaweza ni bora nibaki huku huku ndio pananifaa zaidi,” amesema Mose.
Ameongeza kuwa labda kitu ambacho atakiongeza kukifanya ni kuwa mwalimu na kuwafundisha vijana wengine jinsi ya kucheza.
0 comments:
Post a Comment