Msanii wa muziki wa hip hop One Incredible amedai bado ana ndoto ya kuja
kufanya kazi na msanii mkongwe wa muziki wa hip hop kutoka Marekani,
Eminem.
Rapper huyo alidai wasanii wa hapa nchini ambao alitamani kufanya nao kazi tayari ameshafanya nao kazi.
“Wasanii karibia wote niliotamani kufanya nao kazi nimewamaliza,” One alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio. “Kama ukisema kimataifa ukweli ni msanii mmoja ambaye ni mgumu sana kumpata kwa sababu anaangalia hadi uwezo wako ndiyo muongee , Mungu akijaalia atakuwa Eminem,”
Pamoja na hayo One amewaomba radhi mashabiki zake kwa kuwa kimya muda mrefu na kusema sababu ya ukimya huo kuwa ni kukabiliwa na mambo mengi ya kifamilia huku akiahidi kwamba kwa wakati huu amekwisha yamaliza hivyo ni muda wa kuachia kazi alizokuwa ameziandaa.

0 comments:
Post a Comment