Hatimaye hatua ya raundi ya pili ya robo fainali ya kombe la mabingwa
barani Ulaya (Uefa) iliendelea tena usiku wa Jumanne hii kwa michezo
miwili. Arsenal ambayo ilikuwa katika uwanja wake wa nyumbani Emirates
ilifungwa kwa mara nyingine na Bayern Munich kwa mabao 5-1.
Magoli ya Bayern yalifungwa na Lewandowski dakika ya 55, Robben dakika ya 68, Douglas Costa dakika 78 na Vidal aliyefunga mara mbili dakika ya 80 na 85 huku goli la kufutia machozi la Arsenal likifungwa na Walcot t dakika ya 20.
Na sasa Arsenal imetolewa ikiwa imefungwa jumla ya magoli 10-2 huku ikiwa imejitengenezea rekodi yake kwenye michuano hiyo kwa kuwa kwa miaka ya hivi karibuni haijawahi kufungwa kama hivyo.
Mechi nyingine iliyochezwa usiku huo ilikuwa ni kati ya Napoli waliokuwa katika uwanja wao wa nyumbani, San Paolo ambao walikubali kufungwa na Real Madrid kwa mabao 3-1 na kufanya jumla ya magoli waliyofungwa katika mechi ya kwanza na hiyo kuwa 6-2.
Mechi zingine zinazosubiriwa kwa hamu leo hii ni kati ya Barcelona ambao mechi ya kwanza walifungwa mabao 4-0 dhidi ya PSG na Borussia Dortmund watakao cheza na Benfica ya Ureno

0 comments:
Post a Comment