Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amezionya kampuni za simu kutoweka mazingira ya kuwakwamisha wateja wanaotaka kuhamia mitandao mingine na kwamba watakaobainika kufanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa
Amesema hayo wakati akizindua mfumo mpya wa wateja kuhama mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu. Waziri huyo alisema mtu kuhama mtandao anaoutaka ni jambo la hiari na kuwa kamwe kampuni zisifanye ujanja wa kuweka mazingira ya kukwamisha watu kuhama.
Alisema “Nizionye kampuni zitakazofanya ujanja ujanja wa kuweka mazingira ya kumkwamisha mteja anayetaka kuhama, watakaofanya hivyo tutawachukulia hatua za kisheria, na sitakuwa na huruma maana niko hapa kwa ajili ya maslahi ya Watanzania na tutasimamia sheria kweli kweli.”
Aliongeza “Serikali ya awamu ya tano ina vipaumbele vyake katika sekta ya mawasiliano ikiwamo suala la kuweka mazingira bora ya ushindani katika sekta hiyo ili kuwafanya wananchi kupata huduma ya mawasiliano kwa unafuu.”
Aidha Mbarawa alisema kuanzishwa kwa mfumo huo mbali na kuweka ushindani wa kutoa huduma bora na kupungua kwa gharama za huduma ya mawasiliano, hiyo pia ni njia ya kupima ufanisi wa kampuni za simu
0 comments:
Post a Comment