Kampeni ya ‘Mti Wangu’ ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, itafanyika Jumamosi hii, Oktoba 1
Makonda amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuiunga mkono kampeni hiyo
Faida za miti zipo nyingi sana, tunaamini kwa kipindi hiki tutafikia malengo ambayo tumekuwa tukiyafikiria,” alisema Makonda wakati akiwa katika msafara wake wa zoezi la ukaguzi wa upandaji miti akiongozana na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi.
“Nimshukuru mkuu wa mkoa wa Kinondoni kwa kazi nzuri ambayo ameendelea kuifanya kuniunga mkono, akishirikiana na mkurugenzi wake na wadau wengine na wataalamu wote, kuhakikisha kile ambacho wanaelekezwa wanakifanya kwa uaminifu na kuongeza ubunifu unaoweza kuongeza thamani,” aliongeza.
Pia aliwashukuru watu na makampuni yote yanayomuunga mkono.
0 comments:
Post a Comment