,

,

,

,
Sports

Ndege binafsi ya Cristiano Ronaldo yaanguka



Ndege binafsi ya mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ilianguka wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege wa El Prat jijini Barcelona, Jumatatu. Hakuna majeruhi walioripotiwa.

0f28e1bdc579dff7575c130fe2e1c0077ebe8eff
Kwa mujibu wa ESPN, Ronaldo, aliyekuwa Dortmund kipindi hicho wakati Real Madrid ilikuwa ikijiandaa kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa waliotoka sare ya 2-2 katika hatua ya makundi dhidi ya Borussia Dortmund, hakuwa ndani ya ndege hiyo wakati inaanguka.
Mshambuliaji huyo huikodisha ndege hiyo, Gulfstream G200, aliyoinunua kwa €19m kufanya kazi zingine wakati asipokuwa akiitumia.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Hispania, matairi ya magari hayo yalivunjika wakati ikitua na hivyo kutoka nje ya njia.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.