Msanii wa muziki, Barakah The Prince ameonyesha mafanikio aliyopata kwenye muziki kwa kujenga nyumba kubwa yenye vyumba 5 huku nje akiwa ameweka sehemu ya kuogelea (Swimming Pool)
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Nisamehe’ akiwa amemshirikisha AliKiba, amesema kwa sasa hawezi kuweka wazi gharama ya nyumba hiyo mpaka itakapo kamilika.
“Namshukuru sana mke wangu Naj kwa sababu ana mchango mkubwa sana hadi hapa nilipofika pia kwa sasa siwezi kutaja fedha ambayo nimeitumia hapa kwa sababu ni hela nyingi sana hadi sasa na kama unavyoona nyumba bado haijaisha kwa hiyo nikimaliza kila kitu nitasema ni shilingi ngapi nimetumia,” Barakah The Prince alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Pia msanii huyo aliongeza kwa kusema hivi karibuni anatarajia kufunga ndoa na penzi wake Naj baada tu ya kumaliza mjengo wake huo
0 comments:
Post a Comment