,

,

,

,
AFYA

Faida ya kula siagi yenye karanga

Siagi ya karanga ni moja ya vitu mhimu jikoni katika nyumba nyingi siku hizi, inapendwa na kila mtu watoto na watu wazima. Ukiacha radha yake na tamu, siagi ya karanga ni chakula chenye afya na nguvu.

Hizi ni faida za ulaji wa siagi hiyo:
1. Hukufanya usijisikie njaa kwa muda mrefu
Ni jambo la afya kutumia Siagi ya karanga hasa katika mlo wako wa asubuhi kwa sababu itakufanya ujisikie umeshiba kwa masaa mengi zaidi. Protini na faiba vilivyomo kwenye siagi ya karanga vinaweza kukupunguzia hamu ya kutaka kula vyakula vingine visivyo vya afya au vyakula feki kwa lugha nyepesi.
2. Bora kwa afya ya Moyo
Usawa wa mafuta yasababishayo kolesto ni mdogo sana ukilinganisha na usawa wa yale mafuta yasiyosababisha kolesto katika siagi ya karanga na hivyo kupunguza uwezekano wa mtu kupatwa na matatizo ya moyo. Vitamini E ipatikanayo katika siagi ya karanga ni mhimu sana katika afya ya mfumo wako wa upumuwaji.
3. Siagi ina Mafuta safi
Watu wengi huogopa kutumia siagi ya karanga sababu ya kuwa na kiasi kingi cha mafuta. Lakini ukweli ni kuwa mafuta yaliyomo kwenye siagi ya karanga ni mafuta safi ‘healthy fats’. Asilimia ya mafuta haya yasiyo na kolesto katika siagi ya karanga ni kubwa zaidi na hivyo unaweza kuitumia bila wasiwasi wowote.
4. Ina kiasi kingi cha faiba
Matumizi ya kiasi cha kutosha cha faiba ni mhimu kwa ajili ya ufanyaji kazi mzuri wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Siagi ya karanga ni chanzo kizuri kabisa cha faiba kwa ajili ya mwili.
5. Ina viinilishe vingi mhimu
Siagi ya karanga ina viinilishe vingi na ambavyo ni mhimu sana kwa mwili kama vile faiba, protini, potasiamu, kiuaji sumu, mafuta yenye afya, magnesium na vingine vingi. Viinilishe hivi ni mhimu kwa ajili ya utengenezaji na uimarishaji wa mifupa, kuimarisha mishipa na kuimarisha kinga ya mwili.
6. Huongeza Nguvu
Siagi ya karanga ina kiasi kingi cha mafuta masafi yasiyoweza kusababisha kolesto/lehemu mwilini (unsaturated fats) na kiasi kingi cha protini, vitu hivi viwili vinafanya kazi ya kuongeza nguvu mwilini. Siagi ya karanga ina kalori nyingi zitakazokuwezesha ubaki ni mwenye nguvu kutwa nzima.
7. Huzuia kuzeeka mapema
Kwenye siagi ya karanga kuna kitu kinaitwa kwa kitaalamu ‘resveratrol’. Resveratrol ni kitu mhimu sana katika kuondoa sumu mwilini na hivyo kusaidia kuzuia kansa, matatizo ya moyo na kuzeeka mapema.
8. Huzuia kansa
Uwezo wa siagi ya karanga katika kuondoa sumu mwilini huzuia matokeo ya matendo ya vijidudu nyemelezi vya magonjwa mwilini, wakati faiba kwa uwezo mkubwa husaidia katika kuondoa taka zingine katika mwili hasa kwenye utumbo mdogo na hivyo kuzuia kutokea kwa kansa ya utumbo mdogo.
9. Husaidia mmeng’enyo wa chakula
Siagi ya karanga ina kiasi maridhawa cha vitamin B-3 (Niacin) na manganese vitu ambavyo ni mhimu sana katika kuusaidia mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi vizuri zaidi. Manganizi huvisisimua vimeng’enya mhimu ambavyo vinahusika katika uondowaji wa ammonia mbaya. Manganizi pia huzilinda seli dhidi ya mfadhaiko wa kisakolojia. Niacin ni mhimu sana katika kukuwa na kuendelea kwa seli.
10. Hudhibiti damu sukari
Siagi ya karanga ni mhimu katika kuidhibiti na kuisawazisha damu sukari mwilini kwa sababu ya kiasi kingi cha protini na faiba kilichomo ndani yake.
12. Husaidia katika kujenga mishipa
Kadharika kiasi kingi cha protini kilichomo kwenye siagi ya karanga kinasadikika kuwa na uwezo wa kuongeza nguvu au uwezo wa mwili na kutengeneza mishipa mingi na imara zaidi.
Chanzo: Dk Fadhili Paulo

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.