Klabu ya Yanga imefanikiwa kupata ushindi kwa mara ya kwanza kwenye
mchezo wa ligi kuu Vodacom Tanzania Bara, kwa kuichapa klabu ya Njombe
Mji FC ya mkoani Njombe.
Goli la Yanga limefungwa na Ibrahim Ajib kunako dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo ulioanza kwa kasi.
Kipindi cha pili Njombe Mji walianza kwa kasi lakini hawakufanikiwa kupata goli na mpaka dakika ya 90, Njombe Mji 0 Yanga 1.
Kwa sasa Klabu ya Yanga inakuwa na pointi 4 baada ya kupata sare kwenye mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Lipuli FC, Kwa sasa Yanga wapo sawa na watani wao wa jadi Simba Sports Club, ambao walitoka sare jana dhidi ya Azam FC.
Yanga SC |

0 comments:
Post a Comment