,

,

,

,
Gossip

Lulu Diva adai Wizkid hakuambulia kitu kwake

Msanii wa Bongo Flava, Lulu Diva amekanusha tetesi za kuwahi kutoka kimapenzi na msanii Wizkid kutoka nchini Nigeria.
Hitmaker huyo wa Usimwache na Utamu ambaye kwa sasa ameachia ngoma mpya ‘Give It To Me’, ameiambia Clouds Fm kuwa yeye kukutana na Wizkid ilikuwa ni mipango ya kazi na si vinginevyo. “Alikuwa na special appearance na mimi nilikuwepo siku hiyo na tulipanga mimi na meneja wangu kwa sababu kuna mtu alikuwa anajuana naye alimuita Wizkid pale, kwa hiyo waliongea kuwa tunaenda kukutana kama wasanii na tuliongea kuhusu muziki, so we have fan pale na ikaishia hapo hakukua na kitu kingine,” amesema na kuongeza.
“After party hakuna niliwahi kuondoka tuliongea kuhusu muziki tu…, yeah tutarajie kitu kwa sababu yeye ni msanii na mimi ni msanii hivyo tunaweza tukafanya kitu kizuri zaidi,” amesisitiza.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.