Rapper mkongwe nchini, King Crazy GK amesema akipewa fursa ya kutumia bifu ya Diamond na Alikiba, atawafanya wawe mabilionea.
Rapper huyo amedai kuwa atahakikisha wawili hao wanaongeza uhasama zaidi kuliko hata ilivyo sasa. Wakati mengi yakiendelea kuzungumzwa kila kukicha kuhusiana na wawili hao , GK amesema angewahakikisha wawili hao wanapiga mkwanja wa kutosha.
“Ni upinzani mzuri kama nikipewa mimi kutengeza pesa watakuwa mabilionea wale mabwana,” anasema. “Kwanza nitaongeza conflict, ule mgongano sitoupunguza, nitauongeza, nitazidi kuuvibrate uwe mkubwa watu wa waufeel. Sasa upo upinzani kwa Kiba na Diamond zaidi personal, sasa mimi nitauweka watu wauvae yaani wakikutana pale inakuwa noma,” ameongeza.
Crazy GK anadai angepambana kuwe na mipango ya kuhakikisha wawili hao wanapiga hela nyingi ikiwemo kufanya show uwanja wa taifa
0 comments:
Post a Comment