,

,

,

,
Sports

Drogba akataa kuanzia benchi katika timu yake ya Montreal Impact

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea, Didier Drogba aligoma kuichezea klabu yake ya Montreal Impact katika mchezo wa jumapili baada ya kuambiwa hataanzishwa dhidi ya Toronto ,kulingana na kocha Mauro Biello.

Drogba mwenye umri wa miaka 38 hakuwepo katika uwanja wa michezo wa Saputo ambapo Impact ilipata sare ya 2-2 na hivyobasi kuweza kufuzu kwa michuano ya muondoano ya ligi ya Marekani.
Montreal hapo awali ilikuwa imesema kuwa Drogba alikuwa anauguza jeraha la mgongo na hivyobasi asingeweza kucheza.
Lakini Biello alisema: Hakukubali kwamba angechezeshwa kama mchezaji wa ziada na mwishowe hakutaka kushirikishwa katika kikosi cha watu 18.
Kocha huyo aliongezea: Alikuwa na tatizo katika mgongo wake lakini alikuwa anaweza kucheza.
Drogba amekuwa akitumiwa kama mchezaji wa ziada katika mechi mbili kati ya nne.
Amefunga mabao 10 katika mechi 21 msimu huu.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.