Mchezo wa kusisimua wa ligi kuu ya soka England kati ya majogoo wa London, Liverpool pamoja na mashetani wekundu, Manchester United umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Katika mchezo huo kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa zamu huku kipindi cha pili Liverpool ikishambulia zaidi lango la United.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa hakukasirika lakini pia hakufurahishwa na kiwango cha uchezaji wa timu yake.
Klopp pia ameisifu safu ya ulinzi ya Man U na kusema ilikuwa vigumu kushinda kutokana na ulinzi ulivyokuwa imara.
Kwa upande wake meneja wa Man U Jose Mourinho amesema licha ya kutopata matokeo aliyoyataka lakini ameridhishwa na matokeo hayo.
Katika mchezo huo Ander Herrera aliibuka kuwa mchezaji bora huku mchezaji Paul Pogba akitupiwa lawama na mashabiki wengi kutokana na kiwango chake.
Mfaransa huyo ambaye ada yake ya usajili ilikuwa ni £89 milioni wakati wa majira ya usajili uliopita wa majira ya joto bado hakuonesha thamani yake uwanjani ukilinganisha na kitita kilicholipwa kumnunua
0 comments:
Post a Comment