,

,

,

,
Siasa

Kaka yake Obama kuwa mgeni wa Trump kwenye mdahalo wa tatu wa Urais Marekani

Kaka yake Rais Baraka Obama, mzaliwa wa Kenya, Malik atakuwepo kwenye mdahalo wa tatu na wa mwisho wa Urais wa Jumatano hii kati ya Donald Trump na Hillary Clinton.

Malik — raia wa Marekani anayeishi Washington, DC, anapokuwa nje ya Kenya, amesema atakuwa mgeni wa Trump, mgombea wa chama cha Republican anayemuunga mkono.
“Nina hamu kubwa kuwepo kwenye mdahalo. Trump anaweza kuifanya Marekani bora tena,” Malik aliliambia gazeti la New York Post.
“Ninatazamia kuonana na Malik,” alisema Trump said. “Yupo tofauti na mdogo wake.”

Malik, mwenye miaka mitatu zaidi ya Barack, amesema mara ya mwisho kuonana na Obama ilikuwa ni August 2015 alipotembelea Kenya. Amedai kuwa aliwahi kwenda White House kumsalimia mdogo wake lakini alipata mapokezi ya kawaida mno.
“As usual, it was a hands-off kind of thing, very businesslike, very formal,” alisema Malik.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.