,

,

,

,
Music

Kama ni rahisi kununua tuzo, wanaosema hivyo na wao wakanunue – Babutale

Babutale amezijibu shutuma za baadhi ya mashabiki nchini kuwa wasanii wa WCB wamekuwa wakinunua tuzo

Akiongea na Prince Ramalove wa Kings FM, Tale alikuwa na maneno mafupi tu kuwajibu. “Kama ni rahisi na wao wakanunue,” alisema meneja huyo.
Jumamosi iliyopita Diamond na Harmonize walishinda tuzo za Afrimma zilizofanyika jijini Dallas, Marekani.
Alidai kuwa tuzo hizo ni za Tanzania nzima na imeonesha jinsi gani mashabiki wako nao pamoja. Amesisitiza kwa kuwaomba waendelee kuwapigia kura wasanii wote waliotajwa kwenye tuzo za MTV MAMA wakiwemo wasanii wake wa WCB, Diamond na Raymond.
Wengine ni Alikiba, Navy Kenzo, Yamoto Band na Vanessa Mdee

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.