,

,

,

,
Music

Mandojo na Domokaya wavutiwa na Diamond na AliKiba


Wasanii wa muziki waliowahi kufanya vizuri na wimbo ‘Nikupe Nini’, Mandojo na Domokaya wamemtaja AliKiba na Diamond kuwa ni miongoni mwa wasanii ambao wanatamani kufanya nao kazi

Wakizungumza na On Point ya Clouds FM Jumapili hii, wakali hao wa zamani wamesema kuna wasanii wengi ambao wanatamani kufanya nao kazi.
“Kwanza kabisa sisi kama Mandojo na Domokaya kuna wasanii wengi tunatamani kufanya nao kazi, kama hawa wadogo zetu akina, AliKiba na Diamond. Hawa ni wadogo zetu na wao wanatukubali sana kwa sababu sisi tuliwaanzishia njia kwa hiyo hata sisi tunahitaji kufanya nao kazi ili kuchanganya ladha. Kwa hiyo kuna wasanii wengi ambao tunaweza kufanya nao kazi, Diamond, AliKiba pamoja na wengine,” alisema Mandojo.
Wawili hao ambao wanajipanga kurudi rasmi kweye game,wanafanya bishara ya viatu katika soko la Kariakoo jijini Dar es salaam.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.