,

,

,

,
Music

Meneja wa Alikiba Ajibu Tuhuma za Show ya Mombasa na za Kutunishiana na Wizkid

Aidan Charlie ambaye ni meneja msaidizi kutoka kwenye Menejimenti ya mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba ameongea kuhusu tuhuma mbalimbali zilizotolewa dhidi ya Alikiba kutokana na show ya Mombasa iliyofanyika weekend iliyopita na zifuatazo ni kauli zake

  • Sio kweli kwamba Alikiba alisema yeye ni msanii mkubwa Afrika Mashariki hivyo Wizkid ndio alitakiwa kupanda stejini kabla yake, alietoa hizo habari kadanganya.
  • Kilichotokea ni kwamba kiujumla Waandaaji hawakuwa wamejipanga vyema, show ilitakiwa kuanza saa nane mchana lakini wakaipeleka mbele mpaka saa tatu usiku.
  • Ishu ilikua wakati Chris Brown alipofika kuliangalia jukwaa na kuzoea mazingira ilibidi seti yote ya Alikiba iliyopangwa jukwaani iondolewe pamoja na watu wa Ali, hiyo ikafanya Alikiba achelewe kufanya rehearsal ambapo alimaliza saa mbili usiku na kurudi hotelini kwenda kujiandaa na show.
  • Tumerudi tu hotelini tunapigiwa simu kuambiwa mnatakiwa kupanda kwenye stage ikabidi Alikiba arudi uwanjani lakini muda ulikua umeyoyoma na Chris Brown alitakiwa kutumbuiza mapema ili awahi Airport.
  • Hakuna kutunishiana misuli kokote kati ya Wizkid na Alikiba, wawili hawa wako vizuri na walikua wanaongea backstage na Wizkid alimwambia Ali haondoki uwanjani mpaka aone show yake

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.