,

,

,

,
Gossip

Nataka Kuwa Mcha Mungu, Maisha ya Kuendekeza Dunia Nimeyachoka – Shamsa Ford

Malkia wa filamu na mama wa mtoto mmoja, Shamsa Ford amefunguka kwa kusema kuwa kwa sasa anataka kujikita zaidi kwenye ibada ya kufanya mambo ambayo yanampendeza mwenyezi Mungu.
Shamsa akizungumza baada ya kufunga ndoa


Mwigizaji huyo ametangaza uwamuzi huyo ikiwa ni miezi michache toka afunge ndoa na mfanyabishara wa maduka ya nguo, Chidi Mapenzi.

Maisha ya kuendekeza dunia nimeyachoka. Natamani ifike siku kwa kudra za Mwenyezi Mungu nibadilike. Natamani niwe mmoja ya wale watakaopata nafasi ya kwenda peponi pamoja na familia yangu . natamani nifanye IBADA kama ulivyoamua Mwenyezi Mungu. NATAMANI matendo yangu yawe ya kukufurahisha wewe Mwenyezi Mungu ili umauti utaponikuta niwe msafi..G9T MY PEOPLE. ..INSHAAALLAH MWENYEZI MUNGU ATUPE MWISHO MWEMA. .
Mashabiki wake katika mitandao ya kijamii wameonyesha kupendezwa na uwamuzi huo huku wachache wakimuuliza maswali kama ataendelea kufanya tena filamu.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.