,

,

,

,
News

Sakata la Kuvamiwa Clouds Fm: Clouds Fm waeleza kilichotokea, Waziri Nape kuwatembelea

Weekend hii katika mitandao ya kijamii kimesambaa kipande cha video kinachomwonyesha mtu anayedaiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa na askari wenye mitutu wakiingia kwenye ofisi za kituo cha redio cha Clouds Fm zilizopo Mikocheni Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Live, Ruge Mutahaba
Video hiyo ambayo ilichukuliwa na kamera za CCTV, ilianza kusambaa mitandaoni siku ya Jumamosi asubuhi na kuzua taharuki kwa wananchi wakitaka kujua ni nini kilitokea mjengoni hapo.
Mpaka sasa hakuna taarifa ya jeshi la polisi iliyotelewa kuhusiana na tukio hilo wala RC kufafanua juu ya video hiyo inayosambaa mitandaoni.
Baada ya kusambaa kwa taarifa hiyo, Clouds Fm wametoa taarifa wakieleza nini kilitokea.

Taarifa ya Clouds Fm.


Pia Ruge alisema Jumatatu hii atakuwa live kwenye kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV kuzungumza kuhusu sakata hilo pamoja na mambo mengine.
Katika hali hiyo Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo, Nape Nnuye ametoa taarifa fupi huku akiahidi Jumatatu hii kuwatembelea Clouds Fm.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.