,

,

,

,
Video

VIDEO: Ruge afunguka kuhusu RC Makonda kuvamia Clouds

Mkurugenzi wa Vipindi na Uendeshaji wa Kituo cha Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amefunguka Jumatatu hii katika kipindi Clouds 360 cha Clouds TV na kuthibitisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivamia kituo hicho.
Hayo yametokea baada ya weekend hii kupitia mitandao ya kijamii kusambaa video inamonyesha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akiingia ofisi za Clouds usiku akiwa na askari ambao wana burunduki.
Ruge aliyekuwa akihojiwa na mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast, Masoud Kipanya alisema alipigiwa simu na mmoja wa wafanyakazi wake kuwa Makonda ameingia ofisini hapo akiwa na polisi wenye silaha.
“Jambo hili limeniumiza sana, kwani pamoja na kuwa Makonda ni rafiki yetu lakini hatukutegemea kama angeweza kuingia ofisini na polisi wenye silaha,” alisema na kuongeza
“Hata kama ni rafiki yako, siku moja akiingia nyumbani kwako usiku sana na silaha lazima uhoji.” aliongeza Ruge
                                            ANGALIA VIDEO HAPA CHINI


Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.