Mchezo wa VPL kati ya Mbeya City iliyokuwa mwenyeji wa Simba umemalizika kwa Simba kuendeleza rekodi ya kutokupoteza mchezo wowote kwa msimu wa 2016/2017 na kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
Magoli ya Simba yamefungwa na Ibrahim Ajibu katika dakika ya sita ya mchezo huo kwa kupiga mpira wa faulo uliotinga moja kwa moja nyavuni na goli la pili likifungwa na Shiza Kichuya baada ya kuwapita wachezaji Mbeya City na kupiga mpira ambao uliingia moja kwa moja golini.
Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kusalia kileleni ikiwa na alama 20 na Stand United ikiwa na alama 19 na ikishika nafasi ya pili huku Yanga ikishika nafasi ya tatu na alama 14.