Kama ulidhani Yanga kupoteza mchezo wa Stand United na kutoa sare na Simba kunaonyesha dalili za Yanga kushuka kiwango, bado yawezekana ukawa unakosea kwa kile ambacho wanajangwani hao wameifanyia Mtibwa katika mchezo wa VPL uliopigwa dimba la Uhuru.
Mchezo huo umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushini wa goli 3-1, magoli ya Yanga yamefungwa na Obrey Chirwa dk. 44, Simon Msuva dk. 68 na Donald Ngima katika dakika ya 80 huku goli pekee la Mtibwa likifungwa na Haruna Chanongo dk. 63.
Ushindi ambao wameupata Yanga umewawezesha kufikisha alama 14 na kushika nafasi ya tatu huku ikiwa na michezo miwili ambayo bado haijacheza.