Klabu ya Tottenham Hotspurs inasemekana kuwa ipo tayari kuvunja rekodi yao kwa kutoa kitita cha paundi milioni 40 kwa ajili ya kumsajili Isco kutoka Real Madrid Januari mwakani.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa akihangaika kupata nafasi katika kikosi cha Zinedine Zidane, hadi saivi ameanza katika mechi mbili pekee msimu huu na alikuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Spurs kipindi cha kiangazi.
Madrid wanadaiwa kuwa tayari kumuuza, huku chaguo la kumnasa kwa mkopo na nafasi ya kumnunua moja kwa moja pia ikiwepo.
Isco aliyenunuliwa na Madrid kutoka Malaga miaka mitatu iliyopita tayari ameeleza nia yake ya kuondoka kama atakosa nafasi katika kikosi cha kwanza
0 comments:
Post a Comment