Wizara
ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia ,wazee na watoto inawatangazia
wahitimu wote wa vyuo vikuu vya kada mbalimbali za afya wanaopaswa
kufanywa mafunzo ya utarajali yani ‘internship’ ambao ni madaktari wa
meno, wafamasia, wauguzi, wataalamu wa Radiolojia, wataalamu wa maabara
na wataalamu wa afya ya mazingira kwamba pamoja na kuwa walipaswa kuanza
mafunzo yao leo Oktoba 1, 2016 ambayo ilikuwa ni tarehe rasmi ya
kuanza mafunzo hayo itatangazwa hapo baadae.
Wizara
ya Afya imesema kuwa kuchelewa huko ni kutokana na juhudi zinazoendelea
kufanywa na Wizara ili kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yanaanza katika
namna na mfumo uliobora zaidi.
Aidha
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhammad bakari kambi (Pichani juu)
amesema kuwa mara baada ya juhudi hizo kukamilika wataalamu tajwa
watafahamishwa rasmi na hivyo kuwaomba wataalamu hawa na wadau wengine
kuwa na subira.
“Tunapenda
kuwafahamisha wahitimu ambao walikuwa hawajapangiwa vituo vya kufanyia
mafunzo kwa vitendo, kuwa utaratibu unafanywa kuhakikisha kwamba
wanapangiwa vituo hivi karibuni ambapo mtandao utafunguliwa na wahusika
watapewa taarifa”. Amesema Prof. Muhammad Bakari
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC)
0 comments:
Post a Comment