Ikiwa Jumanne hii ni siku ambayo wanafunzi wa kidato cha nne nchi wanaanza mitihani yao ya taifa, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetoa onyo kwa watu wote watakaojihusisha na vitendo vya udanganyifu
Akiongea na waandishi wa habari Jumatatu hii, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Charles Msonden amesema, “Tunawaasa wanafunzi, walimu na wananchi wote kwa ujumla kutojihusisha kabisa na vitendo vya udanganyifu katika mitihani hii.
“Baraza la mitihani halitasita kumchukulia hatua mtu yoyote atakayejihusisha na udanganyifu katika mitihani kwa mujibu wa wa kanuni za utumishi na sheria za nchi yetu. Ikiwa ni pamoja na kuwafutia matokea watahiniwa wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya udanganyifu,” aliongeza.
Jumla ya watahiniwa 408,442 wamesajiliwa kufanya mitihani hiyo huku wasichana wakiwa ni asilimia 51.28 na wavulana wakiwa ni asilimia 48.72, watahiniwa wa kujitegemea (Private Candidate) wakiwa ni 52,447 na jumla ya shule 4727 zitatumika kufanya mitihani hiyo na vituo 1600 vimeandikishwa kutumika kufanya mitihani hiyo kwa wanafunzi wa kujitegemea.
0 comments:
Post a Comment