Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wametoa pole kwa fimilia ya bondia Thomas Mashali aliyeuawa kwa kupigwa baada ya kupigiwa kelele za mwizi kufuatia ugomvi uliozuka maeneo ya Kimara, jijini Dar es Salaam
Akiongea katika kipindi cha Jahazi Jumatatu hii, Nape amesema tasnia ya michezo imempoteza mtu muhimu ambaye ametangaza nchi kupitia mapigano mbalimbali.
“Tumesikitishwa sana kifo chake ambacho kimetokea kikatili, ni jambo ambalo limetushtua sana kwa sababu tumempoteza mtu muhimu ambaye amefanya kazi kubwa ya kuiwakilisha nchi yetu na kuendeleza tasnia ya ngumu. Kwa hiyo kwa niaba ya serikali natoa pole kwa rais wa chama cha mabondia Tanzania, viongozi, ndugu pamoja na jamaa na marafiki ambao wameguswa kwa namna moja,” alisema Nape.
Mashali aliyezaliwa kwa jina Christopher Fabian Mashale aliuawa baada ya kupigwa akiwa huko Kimara jijini Dar es Salaam. Inasemekana wakati akinywa pombe, ulizuka ugomvi na mtu mmoja ambaye anadaiwa kupiga kelele kusema Mashali ni mwizi na watu kuanza kumshambulia.
Mazishi ya bondia Thomas Mashali yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano kwenye Makaburi ya Kinondoni, Jijini Dsm kuanzia saa 7.00 mchana.
0 comments:
Post a Comment