Staa
wa muziki kutoka Nigeria, Yemi Alade ambaye yupo nchini kwa sasa kwa
ajili ya tamasha la Fiesta Dar 2016, ameeleza jinsi alivyoweza kuimba
wimbo kwa Kiswahili ambao aliupa jina la Na Gode-Swahili Version’.
Akizungumza
na waandishi wa habari kabla ya kufanyika kwa Fiesta, Yemi Alade
amesema anapenda kujifunza lugha mbalimbali ikiwemo kiswahili na
alipotaka kuimba wimbo huo haikumpa shida sana kukamilisha nyimb nzima.
“Napenda
lugha, nina marafiki wanaongea Kifaransa, nina marafiki wanazungumza
Ureno, napenda kujifunza na nilikuwa nikijaribu zaidi na zaidi hadi
nikaweza, kwasasa Vanessa [Mdee] amekuwa akinifunza,” alisema Yemi
Alade.
0 comments:
Post a Comment