HADEMA tunasema hivi, Rais Magufuli
acha mchezo wa kucheza na maisha ya madaktari wetu,
katika mazingira ya
kawaida, ingekuwa wanakwenda Kenya wakati kuna hali ya utulivu, kuna
hali ya uhakika wa Usalama Kenya tungeruhusu vijana wetu wakafanye kazi
kwa sababu hata Wakenya ni ndugu zetu, lakini katika mazingira ambayo
kuna mgomo Kenya, kuna kutoelewana kati ya Serikali ya Kenya na
madaktari wao, sisi ndio tuwe kimbelembele cha kuwatoa watoto wetu
kwenda kutibu Kenya wakati Wakenya wenyewe hawawataki ni kuweka maisha
ya Watanzania wenzetu , wataalam wetu katika risk, sisi Kama Chama Kikuu
cha Upinzani tunapinga, na naomba Mkutano huu Mkuu wa Kanda ya Pwani
utoe tamko la kupinga madaktari wetu kwenda nchini Kenya.
Magufuli na Serikali yake wawape ajira vijana wetu vituo vya afya havina
madaktari, Sera yetu ya Taifa inasema vituo vyetu vya afya lazima
vihudumiwe na madaktari lakini mpaka leo hakuna madaktari kwenye vituo
vya afya kwa sababu Serikali imeshindwa kuajiri.
Kwa hiyo wapo vijana wengi kwa muda wa miaka miwili hawajaajiriwa lakini
suluhu sio kuwakimbizia nchi za jirani ambazo zina migogoro na wataalam
wao, suluhu ni Serikali yetu itafute fedha iwaajiri vijana hawa, mama
zetu, wazee wetu, vijana wetu wanawahaitaji madaktari hawa wawatibu
katika vituo vyetu vya afya katika zahanati zetu katika hospitali zetu,
Kwa hiyo naomba Mkutano Mkuu Maalum wa Kanda Pwani, naomba mnikubalie
Kama Mwenyekiti wa Chama kupitia Mkutano huu tutoe tamko hili rasmi la
kupinga madaktari wetu kwenda nchini Kenya.
0 comments:
Post a Comment