,

,

,

,
Entertainment

Profesa Jay afunguka kuhusu mistari aliyowachana wasanii wenzake kwenye ‘Kibabe'

Rapper na mbunge wa Jimbo la Mikumi, Profesa Jay amefunguka juu ya mistari aliyowachana wasanii wenzake kwenye wimbo wake mpya wa ‘Kibabe’ ambao walikuwa wakipinga ubunge wake wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwkaa 2015.
Katika wimbo huo Jay amewachana kwa kurap, “Nilishawasamehe wasanii wenzangu, waliokuja jimboni kupinga ubunge wangu mabasi na mabasi jiongezeni wanangu. Asante Wanamikumi kwa kuwa na imani kwangu next time mkija tena protect your neck msije mkasema sikusema. Sanaa inataka umoja nitakubeba ukianguka, hao wanawatumia na mwisho wanawatupa.”
Akiongea na kipindi cha Dj Show cha Radio One, Profesa amefafanua kauli hiyo kwa kusema, “Kuna baadhi ya wasanii walikuja wakanisupport lakini kuna wengine walikuja Mikumi pia walikuwa wakisupport upande mwingine, kitu nilichojaribu kukisema hapo tunajua wasanii walikuwa kazini lakini kitendo chao cha kunipinga mimi kuungwa wanajisikia vibaya sana.”
“Wengi nimekuwa nikikutana nao wamekuwa hawana amani. Maana yangu ilikuwa ni kutoa kama statement hivi kwamba najua mlikuja, najua mnajisikia vibaya, najua mlikuwa kazini lakini kilichofanya tukawa tofauti naamini kabisa kuna kesho na kesho kutwa kwamba ukidondoka wewe mimi naweza nikakusupport bado naamini hiki, sisi ni ndugu ingawa tupo kwenye itikadi tofauti,” ameongeza.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.