Msanii Shilole ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Sitoi kiki'
amefunguka na kuwataja wasanii watano wa bongo fleva ambao yeye
anawakubali na kupenda kazi zao.
Shilole alifunguka hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa
Radio na kusema katika wasanii hao msanii wa kwanza kabisa anayemkubali
ni Bi. Khadja Kopa
"Jamanii mimi nampenda sana huyu mama Khadja Kopa, nampenda sana sana
lakini mbali na huyo pia napenda kazi za msanii Linah Sanga, Mwasiti,
Diamond Platnumz pamoja na huyo kijana huyu ambaye ameniimba, anaitwaa
RayVanny" alisema Shilole
Mbali na hilo Shilole anasema hakubatika kwenda kwenye harusi ya Nuh
Mziwanda sababu alikuwa na mishe zake zingine lakini amedai siku ya
arobaini ya mtoto wake atakwenda kumuona mtoto na kumpa pongezi kwa
kubarikiwa kupata mtoto.
0 comments:
Post a Comment