Huyu Ndugu Makonda. Ni vile wengi hawamfaham. Kama akiwa rafiki yako,
akiwa chini yako hutaacha kumpenda. Ni mtu ambaye unapompa maelekezo
anasikiliza. Anafanya kwa namna ambayo unataka iwe.
Bwana makonda ni mtu ambaye kama amelala ukamwamsha kuwa tukachote maji
ndoo mbili mbili atakuuliza kwa nini tusichote nne? Au ukichota mbili
ukapumzika yeye ataendelea kuchota zaidi. Kwa nini usimpende. Ni aina ya
mtu ambaye when you tell him. Jump! He will ask "how high? Kwa
unyenyekevu kabisa. Ukimwambia akimbie mita 100 atakimbia 1000.
Ungemuuliza Marehem Sitah angekwambia. Ungemuuliza Riziwan angekwambia
kuwa This man ni mtiifu sana. Ni msikivu unapompa maelekezo hufuata bila
kusita, bila kuuliza uliza. Ni kwa nini usimpende?
Akiwa rafiki yako. Ikatokea ukamfahamisha kwa baba yako. Atamheshimu
baba yako, atampenda na kumjali.wakat wewe hupigi simu mpaka uwe na
shida. Yeye atapiga simu na kumuuliza " mzee habari za asubuh?umeaamkaje
hajambo na mama? Haya mi nlikuwa nawasilimia tu. Mungu awabariki" kwa
nini mzee wako asimpende? Asitaman awe mtoto wake?
Jamaa anachapa kazi. Akipewa kazi anafanya hasa. Ni aina ya watu ambao
husemwa "amesifiwa kukimbia kapitiliza hadi kwao" anafanya kazi kwa
kujituma sana.
Alipoambiwa adui mkubwa wa CCM ni Ed Lowasa alipambana na Lowasa mchana
na usiku. Alimtukana na kumkebehi.aliambiwa yeye adeal na lowasa
akafanya kaz kwa mapenz makubwa sana wakamwona anafaa.
Akaambiwa sasa ahamishie nguvu zote kwenye katiba mpya. Aipinge mchana
na usiku. Alifanikiwa sana na tunajua nini kilitokea kwa mzee warioba
kwenye mkutano wake wa mwisho pale udsm.
Sasa mtu wa hivi kwa nini asipendwe?kwa nini asiaminiwe?ni mwaminifu na
mtiifu. Haulizi maswali. Anasema hewala baba ntafanya. Vijana wengine
wanahoji. Wanasema hili haliwezekani. Wakati yeye haamini kama kuna
jambo ataambiwa haliwezekani.kwa nini asipendwe?
Kila chama ili kisimame kinahitaji akina yeye. Hawa ni watu wa muhimu
sana katika ujenz wa chama na hata serikalini. Hutumika na watawala
sehemu yoyote il duniani wanakuwepo. Hawa hutenda kwa uaminifu yale
watawala wanayotaka yatokee.ni waaminifu sana. Adolf hitler alikuwa nao,
idd amini alikuwa nao, bokassa alikuwa nao, djamen alikuwa nao, nyerere
alikuwa nao, mandela alikuwa nao. Kila kiongozi anakuwa nao. Ni watu
muhimu sana kushikilia itikadi.
Ni vile hamjamfaham makonda mkimfaham hata ninyi mtampenda. Mtatamani
kumsajili awe kwenu. Trust me kama ingekuwa kunafanyika usajili basi
angekuwa anagombaniwa kwa dau kubwa sana.
Hayo ni maoni ya mmoja wa wasomaji wetu
0 comments:
Post a Comment