,

,

,

,
Siasa

Polepole amkingia kifua Kinana

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amekanusha taarifa zinazovumishwa katika mitandao ya kijamii, kwamba Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, John Magufuli amebadili baadhi ya vipengele vya katiba ya CCM ili apite bila kupingwa na wajumbe wa Kamati Kuu (NEC) ya chama hicho, katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya urais kupitia chama hicho mwaka 2020.

Polepole ameyasema hayo Machi 26,2017 wakati akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam.
Ameeleza kuwa, “Machi 12, 2017 tulifanya mabadiliko ya katiba yanayohusu utaratibu wa ugombea urais na mchakato wa kumpata mgombea urais wa chama, lakini watu wachache wanatumia taarifa hiyo kupotosha kwamba rais Magufuli hatokuwa na mgombea mwenza ndani ya chama katika kugombea nafasi ya kukiwakilisha chama ngazi ya urais mwaka 2020.”
Licha ya hayo, Polepole amesema amesikitishwa na taarifa zilizosambazwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii, kuwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alizuiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari, na kusema kwamba Kinana yuko kwenye matibabu hivyo hali yake kiafya ikitengemaa atarejea katika majukumu yake.
“Kama kuna taarifa hamuielewi ni vyema mkawatafuta wasemaji wa chama kwa ufafanuzi zaidi, si vyema kuwaletea taharuki wanachama na watanzania kwa ujumla kwa kuwapa taarifa za uongo,” amesema na kuongeza.
“Tunaheshimu uhuru wa watu kutoa maoni yao kwa mujibu wa katiba ya nchi, ila tunahudhunishwa na watu wachache wenye nia ovu ambao hupotosha taarifa za nchi na chama. Tunawaomba wanachama na umma kwa ujumla kupuuza taarifa hizi sababu zina lengo la upotoshaji,” amesema.

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.